Na. Dennis Gondwe,
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma inajenga vituo vya afya maeneo ya kimkakati ili kuwafikishia huduma wananchi wengi zaidi na kuwaondolea kero ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya jijini humo.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alipoongoza Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya jiji hilo kutembelea ujenzi wa vituo vya afya unaoendelea.
Mkurugenzi Mafuru alisema kuwa uchaguzi wa maeneo ya kujenga vituo vya afya katika halmashauri yake unaangalia wingi wa wananchi. “Mtaona kuwa uamuzi wa kujenga kituo cha Afya Chang’ombe eneo hili ulikuwa sahihi. Eneo hili ni la kimkakati kwa sababu lina watu wengi na hakuna kituo cha afya jirani. Wananchi wamekuwa wakisafiri kufuata huduma za afya katika kituo cha Afya Makole ambapo ni mbali” alisema Mafuru.
Alisema kuwa lengo la ujenzi wa vituo vya afya na mtawanyiko wake ni kuwasogezea huduma za afya wananchi wake kama yalivyo malengo ya serikali ya awamu ya sita.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.