Na Noelina Kimolo, DODOMA
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeishukuru benki ya Exim kwa msaada wa wadawati 50 yaliyotolewa na benki hiyo kama mdau wa elimu kwa lengo kuboresha miundombinu na mazingira ya kujifunzia Jijini humo.
Shukrani hizo zimetolewa na Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri hiyo, Joseph Mabeyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya madawati hayo iliyofanyika katika ofisi za Jiji hilo Julai 5, 2021.
Afisa Elimu huyo alisema kuwa madawati hayo yatasaidika katika kupunguza tatizo la upungufu wa madawati kwenye shule za msingi.
“Madawati haya tuliyopokea leo naamini yatatusaidia kupunguza changamoto ya madawati kwa kiasi kikubwa kwa wanafunzi wa shule ya msingi waliopo kata ya Hombolo Bwawani” alisema Mabeyo.
Aidha, Afisa Elimu huyo alimpongeza Mbunge wa jimbo la Dodoma Antony Mavunde kwa ushirikiano mkubwa anao uonesha kwa kutafuta wadau wengi ili kuendelea kuleta maendeleo katika sekta ya Elimu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa benki ya Exim, Agnes Kaganda alisema kuwa benki hiyo imekuwa na utaratibu wa kutoa misaada ya madawati katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuinua nakuboresha elimu.
“Sisi tumeamua kuwa sehemu ya upungufu huo kwa kutatua tatizo la madawati kwa wanafunzi wa shule za msingi, tupo hapa kwa ajili ya kukabidhi madawati 50 ambayo yatatumiwa na wanafunzi 200 hivyo kwa kiasi Fulani tutakuwa tumepunguza changamoto ya wanafunzi kukosa mawadawati” alisema Kaganda.
Pia, Kawanda alisisitiza ushirikiano huo uendelee ikiwa ni njia kubwa ya kuleta umoja na mshikamano katika kulijenga Taifa la Tanzania.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.