HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeahidi kutunza msaada wa mashine mbili zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni saba za kuwasaidia wagonjwa kupumua na kuratibu mapigo ya moyo ili zidumu na kunufaisha wagonjwa wengi zaidi.
Kauli hiyo ilitolewa na Mganga mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Gatete Mahava baada ya kupokea mashine mbili za kuwasaidia wagonjwa kupumua kutoka shirika la Jhpiego ofisini kwake.
Dkt. Mahava alisema “leo tumepokea mashine mbili ‘Pulse Oximeter’ na ‘Oxygen Concentrator’. Mashine hizi zinasaidia kwa watu wenye shida ya upumuaji na kuangalia mapigo yao ya moyo yanavyofanya kazi na kupima ‘concentration’ ya ‘oxyegen’ kwenye mwili wao”.
Mashine hizi zitasaidia wagonjwa wote wenye matatizo ya kupumua, aliongeza.
“Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, tunatoa shukrani za dhati na kwa niaba ya wananchi wa Dodoma kwa uongozi wa Jhpiego makao makuu kwa kutupatia mashine hizi muhimu. Tunaahidi kuzitunza mashine hizi ili zidumu na kuhudumia wagonjwa wengi zaidi katika Jiji letu” alisema Mganga mkuu huyo.
Kwa upande wake mwakilishi wa shirika la Jhpiego, Isabella Neeso alisema “nimekuja hapa kukabidhi msaada ambao tumeona utawezesha kusaidia kuboresha huduma za afya kwa Jiji la Dodoma. Msaada huu una gharama ya zaidi ya shilingi Milioni saba na tumeupata kupitia mdau wetu ambae anaitwa EJAF. Mdau huyu ameona ni vizuri Jiji likipata mashine mbili zitakazoweza kusadia kuboresha huduma za matibabu. Tutaendelea kutoa misaada kadiri itakavyopatikana na ikibidi tutaangalia maeneo ya kuendelea kuboresha huduma” alisema Neeso.
Mwakilishi wa shirika la Jhpiego, Isabella Neeso (kushoto) akimkabidhi Mganga mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Gatete Mahava (kulia) machine ambazo zimetolewa leo ofisini kwa Mganga Mkuu wa Jiji.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.