Na. Dennis Gondwe, DODOMA
Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imekadiria kukusanya na kutumia mapato yenye jumla ya shilingi 128,278,555,369 kutoka vyanzo katika vyanzo vyake vya ndani, serikali kuu, wahisani kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo, utoaji huduma na kujiendesha.
Kauli hiyo ilitolewa na Mchumi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Francis Kaunda alipokuwa akiwasilisha makadirio ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Dodoma.
Kaunda alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imekadiria kukusanya na kutumia mapato yenye jumla ya shilingi 128,278,555,369 kutoka vyanzo katika vyanzo vyake vya ndani, serikali kuu, wahisani kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo, utoaji huduma na kujiendesha.
Akiongelea sura ya Mpango na Bajeti ya mwaka 2023/2024 “mapato ya ndani ni shilingi 55,128,229,369 na matumizi ya ruzuku ya mishahara ni shilingi 59,082,835,000. Ruzuku ya matumizi mengineyo shilingi 1,005,792,000 na matumizi ya ruzuku ya miradi ya maendeleo ni shilingi 13,061,699,000” alisema Kaunda.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.