KAMA ilivyo ada ya kufanya usafi, Halmashauri ya Jiji la Dodoma kupitia Idara ya Usafi wa Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu, Jumamosi ya leo wamefanya ukaguzi wa mifumo ya maji taka katika Kata ya Uhuru.
Akiongea na tovuti hii Dickson Kimaro ambaye ni mkuu wa Idara hiyo amesema wananchi wanapaswa kutunza mazingira yao na kuhakikisha mifumo ya maji taka inafanya kazi vizuri ili kuepuka kero ya harufu na magonjwa ya kuambukiza na hata uchafuzi wa mazingira.
Mkuu huyo wa Idara ya Mazingira ametahadharisha kuwa yeyote atakayekutwa ameunganisha mfumo wa maji taka kwenye mfumo wa maji ya mvua atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kuondoa uchafu aliousababisha na kulipa faini ya uchafuzi wa mazingira na uharibifu wa miundombinu husika. Amesema jukumu la kulifanya Jiji kuwa safi ni la kila mmoja, na kila mtu anatakiwa kuwa mlinzi na mshauri wa mwenzie ili kwa pamoja kuweka mazingira safi na salama kwa mustakabali wa afya za wananchi wa jiji la Dodoma.
Aidha amewataka wananchi wenye uhitaji au kuwa na changamoto ya maji taka kuwasiliana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) ili waweze kuunganishwa kwenye mfumo mkuu wa maji taka.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.