Halmshauri ya Jiji la Dodoma imeibuka mshindi wa kwanza katika maonesho ya Wakulima maarufu kama Nanenane kwa kundi la Halmashauri za Mkoa wa Dodoma, ambapo imezishinda Halmashauri nyingine saba za Mkoa huo ambazo ni, Mpwapwa, Kongwa, Chamwino, Bahi, Chemba, Kondoa, na Kondoa Mji.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira Anthony Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma akitazama bidhaa za Wakulima na Wajasiriamali katika Banda la Jiji la Dodoma wakati wa Maonesho ya Wakulima Nanenane Kanda ya Kati katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma. Nyuma kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi na kushoto ni Meya wa Jiji la Dodoma Mstahiki Profesa Devis Mwamfupe.
Kufuatia ushindi huo, Kamati ya maandalizi ya maonesho hayo kwa Mikoa ya Kanda ya Kati ililikabidhi Jiji la Dodoma Cheti cha mshindi wa kwanza wa maonesho hayo ambayo yalifikia tamati Agosti 8 mwaka huu katika Viwanja vya Nzuguni Jijini humo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira Anthony Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma (wa pili kulia) akitazama bidhaa za Wakulima na Wajasiriamali katika Banda la Jiji la Dodoma wakati wa Maonesho ya Wakulima Nanenane Kanda ya Kati katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi.
Maonesho ya Wakulima Nanenane hufanyika kila mwaka kuanzia Agosti Mosi na kufikia kilele Agosti 8, ambapo lengo kuu limekuwa ni kutoa Elimu na kubadilishana uzoefu miongoni mwa Wakulima ili kuboresha uzalishaji na kuinua uchumi wao na Taifa kupitia Kilimo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.