HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeweka mkakati wa kuondoa daraja la sifuri 'zero' katika matokeo ya mitihani ya kitaifa kwa wanafunzi wa shule za sekondari.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Elimu ya Sekondari katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Martin Nkwabi katika kikao kazi kilichohusisha wataalam wa idara ya elimu sekondari wa Halmashauri ya Jiji, wakuu wa shule zote za sekondari na maafisa elimu Kata; na kufanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Dodoma.
Wakati akifungua kikao kazi hicho, Nkwabi alisema kuwa kinalenga kuweka mbinu na mikakati itakayosaidia kuboresha ufundishaji na kuinua zaidi ufaulu kwa shule za sekondari za Halmashauri ya Jiji la Dodoma. "Kama mwaka huu imewezekana kwa shule ya sekondari Dodoma kutokuwa na 'four' au 'zero' basi moto huu tuuendeleze kwenye shule zote za sekondari za Jiji letu, na hilo linawezekana kama kwa pamoja tutachapa kazi" alisema Nkwabi.
Akiongelea suala la upandishaji madaraja kwa walimu, mkuu huyo wa idara ya elimu sekondari alisema kuwa suala hilo linaendelea kushughulikiwa na Halmashauri likiwa katika hatua nzuri ya utekelezaji. Alisema kuwa wakati serikali ikiendelea kufanyia kazi suala la madaraja, walimu wanawajibu wa kutekeleza majukumu yao kwa viwango vya juu ili kufikia malengo ya elimu ya Halmashauri.
Kikao kazi hicho kiliazimia kufuta daraja sifuri kwa shule zote za sekondari katika Halmashauri hiyo na kuanzisha makambi ya kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha Nne. Azimio lingine lilikuwa ni kuinua kiwango cha uwajibikaji kwa walimu wote katika Halmashauri.
Ikumbukwe kuwa katika matokeo ya mtihani wa kumaliza kidato cha sita shule ya sekondari ya Dodoma ilifaulisha kwa kiwango cha daraja la I, II na III tu.
Afisa Elimu Sekondari wa Jiji la Dodoma Martin Nkwambi (mwenye suti nyeusi) akiongoza kikao kazi kupanga mikakati wa kuhakikisha ufaulu unapanda katika jiji la Dodoma. Aliyesimama kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Dodoma akiwakaribisha wajumbe wa kikao hicho kilichofanyika tarehe 24/07/2019 katika ukumbi wa mikutano wa Shule ya Sekondari Dodoma.
Watumishi wa Idara ya Sekondari, Maafisa Elimu Kata na Wakuu wa Shule za Sekondari za Jiji la Dodoma wakishiriki kikao kazi cha kuweka mkakati wa kuboresha elimu na kuinua ufaulu kwa shule za sekondari za Jiji la Dodoma.
Watumishi wa Idara ya Sekondari, Maafisa Elimu Kata na Wakuu wa Shule za Sekondari za Jiji la Dodoma wakishiriki kikao kazi cha kuweka mkakati wa kuboresha elimu na kuinua ufaulu kwa shule za sekondari za Jiji la Dodoma.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Viwanjani Kaizirege Adelifi akichangia mada wakati wa kikao kazi cha kuweka mkakati wa kuboresha elimu na kuinua ufaulu kwa shule za sekondari za Jiji la Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.