HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imetangaza fursa za uwekezaji katika kituo kikuu cha kuegesha magari makubwa ya mizigo kilichopo Nala kwa wawekezaji mbalimbali kuwekeza katika kituo hicho.
Kauli hiyo ilitolewa na Mchumi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Fred Robert alipokuwa akiwasilisha mada juu ya fursa za uwekezaji katika Jiji la Dodoma kwenye mkutano wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (Tanzania Private sector breakfast meeting) uliofanyika katika hoteli ya Dar es Salaam Serena.
Robert alisem kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma imekamilisha ujenzi wa kituo kikubwa kwa ajili ya maegesho ya magari makubwa ya kusafirishia mizigo katika eneo la Nala.
Akiongelea fursa zilizopo katika kutuo hicho, alisema kuwa vipo viwanja vilivyopimwa kuzunguka eneo hilo. “Fursa zilizopo ni viwanja kwa ajili ya ujenzi wa maghala kwa ajili ya kupakilia, kushushia na kuhifadhia mizigo. Fursa ya kujenga nyumba za kulala wageni na migahawa kuzunguka kituo cha kuegesha magari makubwa ya mizigo” alisema Robert.
Fursa nyingine katika eneo hilo alizitaja kuwa ni maduka mbalimbali ya vipuli na bidhaa za rejareja. Nyingine ni maeneo kwa ajili ya matengezo ya magari na maeneo ya kuoshea magari, aliongeza.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF), Zachy Mbenna amesifu uwekezaji huo wa miradi ya kimkakati ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma na ameshukuru Jiji kuona umuhimu wa kuwatembelea katika mkutano wao, "tutashirikiana kufanikisha hili" alisema Mbenna.
Baadhi ya picha za eneo la uegeshea malari Nala
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.