Halmashauri ya Jiji la Dodoma imetoa msaada wa vitu mbalimbali kumsaidia mama aliyejifungua watoto watatu Yasin, Yasir na Yusira (miezi 3) katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Dodoma Mjini St. Gemma hivi karibuni.
Hatua hiyo imekuja baada ya Hawa Omary Juma (26) kuandika barua kwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuomba msaada kwa kuwa familia yao haimudu kuwalea watoto hao waliozaliwa kwa pamoja.
Akikabidhi mahitaji hayo Afisa Ustawi wa Jamii wa Jiji la Dodoma Bi Rebeka Ndaki amesema Halmashauri imeona umuhimu wa kumsaidia huyu mama baada ya kupokea barua ya kuomba msaada.
“Baada ya kupokea barua ya huyu mama tuliamua kumsaidia maana moja ya majukumu yetu ni kusaidia watu wenye mahitaji maalum kama huyu mama” Alisema Rebeka.
Mahitaji yaliyotolewa ni pamoja na maziwa ya watoto wachanga, mifuko ya sabuni, Pampasi, Sukari na mafuta ya kupaka, vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya laki 4.
Kaimu Mtendaji wa Kata ya Changombe Bi Rebeka Haule alitoa wito kwa wakazi wa Jiji la Dodoma zikiwemo taasisi mbalimbali za misaada ya kiutu na taasisi za dini kujitokeza kuisaidia familia hii kwa kuwa watoto ni baraka kutoka kwa Mungu.
Hawa Omary Juma ni mama wa watoto sita (6) tayari ana watoto wengine watatu anaowahudumia ambao ni Hadija Idd Abdallah (8), Ahmad Idd Abdallah (5) na Mariam Idd Abdallah (3) na anaishi na mume wake ambaye ni dereva wa bodaboda mtaa wa Mtakuja kata ya Changombe Jijini Dodoma.
Hawa Juma (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii wa Jiji la Dodoma ambao wamewapakata watoto wa Hawa walipomtembelea nyumbani kwake Chang'ombe kumpa misaada ya kijamii na kumpongeza kwa kujaliwa kupata watoto mapacha watatu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.