Na. Dennis Gondwe, DODOMA
KITUO cha Afya Nkuhungu kilipokea kiasi cha shilingi 167,000,000 mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya ujenzi wake ili kiweze kuhudumia wananchi zaidi ya 10,000 katika Jiji la Dodoma.
Kauli hiyo ilitolewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Andrew Method alipokuwa akitoa taarifa fupi ya ujenzi wa kituo cha Afya Nkuhungu kwa Timu ya Menejimenti ya halmashauri hiyo ilipofanya ziara ya kawaida ya kutembelea maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho mwishoni mwa wiki.
Dkt. Method alisema kuwa kituo hicho kilipokea shilingi 167,000,000 kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji kwa ajili ya ujenzi wa majengo mawili. Jengo la wagonjwa wa nje na jengo la maabara, jengo yote yapo hatua ya renta alisema.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.