TIMU ya menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaheshimu maoni na ushauri wa Mkaguzi wa Ndani katika kujenga halmashauri inayowajibika katika matumizi ya fedha.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alipokuwa akijibu maswali na hoja mbalimbali za waheshimiwa madiwani katika mkutano maalum wa Baraza la Madiwani alipokuwa akifafanua na kujibu hoja za madiwani katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mafuru akijibu hoja iliyotolewa na Diwani wa Kata ya Chang’ombe, Mhe. Bakari Fundikira kuhusu kujibu hoja za ukaguzi. Mkurugenzi Mafuru alisema “Sisi timu ya menejimenti tunaheshimu sana maoni na maelekezo ya Mkaguzi wa Ndani. Kimsingi tumemuacha huru sana hapa jiji ili aseme na kuandika chochote ili halmashauri twende pamoja, kuliko kumtisha tisha akaficha vitu na vikaibuliwa na CAG inakuwa mbaya sana”.
Akijibu hoja ya Diwani wa Kata ya Makutupora, Mhe. Elia Lenjila, aliyetaka utekelezaji wa maagizo ya baraza kukamilisha miradi viporo ya halmashauri. Mkurugenzi alisema kuwa halmashauri imetekeleza agizo hilo. “Ukienda kwenye bajeti yetu, miradi viporo yote ndiyo imetangulia. Tunatamani ikifika Julai mwakani tunapofanya tathmini tusikute tuna miradi kiporo” alisema Mkurugenzi Mafuru.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.