Na. Dennis Gondwe, DODOMA
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imepanga kukamilisha ujenzi wa kituo cha Afya Kizota ili kiweze kuhudumia wakazi zaidi ya 15,000.
Kauli hiyo ilitolewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Andrew Method alipokuwa akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya Kizota kwa Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilipotembelea kituo hicho kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho mwishoni mwa wiki.
Dkt. Method alisema kuwa ujenzi wa kituo cha afya unaendelea vizuri na kitakapokamilika kinatarajiwa kuhudumia wananchi zaidi ya 15,000. “Kituo kinajengwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Kiasi cha shilingi 167,000,000 kilitolewa na Halmashauri kwa ajili ya ujenzi” alisema Dkt. Method.
Akiongelea mipango ya kukamilisha kituo hicho, alisema kuwa kinatarajiwa kukamilika mapema ili mwaka wa fedha unapoanza kianze kutoa huduma. Vilevile, Halmashauri inaangalia utaratibu wa kujenga mfumo wa kuvuna maji ya mvua ili kukalibiana na changamoto ya maji, aliongeza.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.