HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zimeanza programu ya kutoa Elimu ya Kodi kwa Wafanyabiashara na Wananchi wote Jijini Dodoma, ikiwa ni moja ya mikakati ya kuhakikisha kila muhusika analipa kodi bila shuruti kwa manufaa ya Taifa.
Mkuu wa Idara ya Fedha na Biashara wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Alfred Mlowe amesema zoezi hilo litafanywa na Mamlaka hizo kwa siku nne kuanzia leo Jumanne Oktoba 2, 2018, hadi Ijumaa Oktoba 5, 2018 katika viwanja vya Nyerere vilivyopo katikati ya Jiji hilo.
Alisema lengo la mpango huo ni kuziwezesha Mamlaka hizo kukutana na wadau, ambao wengi ni wafanyabiashara mbalimbali ili kuwaongezea uelewa wa masuala ya kodi pamoja na kukumbushana haki na wajibu ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa kodi mbalimbali, hali itakayosaidia kuongeza uwezo wa Halmashauri na Serikali kwa ujumla kutekeleza miradi ya maendeleo kwa manufaa ya Wananchi ambao ndiyo walipakodi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.