Na Josephina Kayugwa, Dodoma
DIWANI wa kata ya Mpunguzi Jijini Dodoma Mh. Innocent Nyambuya amesema Wananchi wote wa Dodoma wanatakiwa kujilinda na kuwalinda wengine kwa kutoa elimu na kukumbusha jinsi tutakavyoweza kujilinda dhidi ya ugonjwa wa kichaa cha Mbwa.
Alitoa kauli hiyo leo tarehe 28 Septemba, 2022 katika maadhimisho ya siku ya kichaa cha Mbwa Duniani ambapo kitaifa yamefanyika katika Kata ya Mpunguzi Jijini Dodoma na kauli mbiu isemayo "Kichaa cha Mbwa, vifo sifuri".
"Wakazi wote wa Mpunguzi mnatakiwa kuwapatia chanjo wanyama wenu ili tuweze kujilinda na ugonjwa huu wa kichaa cha Mbwa ambao hauna tiba na njia pekee ya kujilinda ni kuchanja wanyama wote wenye uwezo wa kueneza ugonjwa huu hasa paka na Mbwa.
"Na kila mtu ambaye anafuga mfugo wa aina yoyote anatakiwa kumuweka mahali salama ili asizurure hivyo na kuleta madhara kwa binadamu na wanyama wengine kwasababu jukumu na kulindana ni letu sote," alisema Nyambuya.
Kwa upande wake Nasoni Kenesi, mkazi wa kaya ya Mpunguzi ameishukuru Serikali kwa kuwapa elimu juu ya umuhimu wa kuchanja mifugo hasa Mbwa na Paka ambao wana uwezo mkubwa wa kueneza ugonjwa wa kichaa cha Mbwa.
"Kiukweli elimu hii itatusaidia na tutajilinda sote dhidi ya ugonjwa huu kwa sababu umekuwa ukituletea madhara makubwa sana, kwa hiyo wananchi wote wapeleke mifugo yao ikapatiwe chanjo ya kichaa cha Mbwa.
"Kama sheria ipo itumike au kuwepo na adhabu kwa mtu ambaye atakuwa hajamchanja mnyama wake, na mifugo yote inayozurura hivyo tunaomba Serikali itusaidie jinsi gani ya kuipunguza maana imekuwa ikileta madhara,"alisema Keseni.
Kila Mwaka maadhimisho ya kichaa cha Mbwa hufanyika tarehe 28 Septemba, 2022 na maadhimisho haya yalianza tarehe 26 Septemba na kazi za udhibiti wa kichaa cha mbwa kwa mfumo wa kampeni zitaendelea mpaka tarehe 02 Oktoba, 2022.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.