RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wote wenye sifa kujiandikisha kwenye Orodha ya Wapiga kura wa Serikali za Mitaa utakaofanyika nchi nzima Oktoba 11-20, 2024.
Mhe. Dkt. Samia ameyasema hayo leo wakati alihutubia wananchi wa Halmashauri ya Wilaya Nyasa mkoani Ruvuma katika mkutano uliofanyika viwanja vya Bandari ya Mbambabay.
Amesema ili uwe mpigakura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 ni lazima uwe umejiandikisha kwenye Orodha ya Wapigakura wa Serikali za Mitaa ambapo zoezi hilo litafanyika kuanzia tarehe 11-20/10/2024 nchi nzima na uandikishaji utafanyika kwenye vijiji/vitongoji pamoja na mitaa.
“Hivyo niwaombe wananchi wote wenye sifa muda ukifika mkajiandikishe, hili daftari la Kudumu la Wapigakura linaloendelea hivi sasa kwenye maeneo mbalimbali ni kwa ajili ya uchaguzi wa Madiwani, Wabunge na Rais utakaofanyika mwaka 2025 ila kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 mnatakiwa wote mkajiandikishe kwenye mitaa yenu,” amesisitiza
Aidha amewataka wananchi wote kutunza amani na utulivu wakati wote wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na kuhakikisha wanachagua viongozi waadilifu watakaowaletea maendeleo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.