Na: James Mwanamyoto-OR-TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa alisema hatosita kumchukulia hatua Mkurugenzi yeyote wa Halmashauri ambaye atabainika kushindwa kutekeleza kikamilifu ujenzi wa miradi ya miundombinu ya afya ili kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.
Mchengerwa alisema hayo leo wakati wa kikao kazi na watumishi wa Idara ya Afya, ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais-TAMISEMI kilicholenga kujadili utekelezaji wa majukumu ya idara hiyo pamoja na kuhimiza uwajibikaji.
Alisema kuwa, kama kuna halmashauri imepelekewa fedha na kubainika kushindwa kukamilisha kikamilifu ujenzi wa miradi ya miundombinu ya afya, hatosita kumsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi.
"Nipatieni orodha ya wote walioshindwa kukamilisha miradi, wabadhilifu wa fedha za miradi, waliojenga chini ya kiwango na wale ambao wamepelewa fedha lakini bado zipo kwenye akaunti ili niwachukulie hatua za kinidhamu bila kuchelewa," alisema Mchengerwa.
Aidha, aliwataka watendaji wa ofisi yake kushirikiana na wawakilishi wa wananchi katika kubaini maeneo ya kujenga miradi ya miundombinu ya afya kulingana na uhitaji.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.