MADAKTARI bingwa wa upasuaji wa moyo, mishipa ya damu na kifua wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kutoka kwenye mshipa wa damu wa kifuani na kupeleka kwenye mishipa ya damu ya miguuni (Axillobifemoral Bypass Graft Surgery).
Upasuaji huo ni wa kwanza kufanyika hapa nchini ambapo mgonjwa alikuwa na tatizo la kupata maumivu makali maeneo ya miguuni, mapaja na sehemu ya kukalia kwa muda wa miezi nane, baada ya uchunguzi ikagundulika mshipa wake mkubwa wa damu (Abdominal Aorta) umeziba kabisa na hivyo kushindwa kupeleka damu kwenye miguu (Aortoilliac Occlusion Disease) damu ilikuwa inapelekwa kupitia mishipa midogo (Collaterals).
Akizungumza daktari bingwa wa upasuaji wa moyo, mishipa ya damu na kifua wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Alex Joseph amesema walimpokea mgonjwa huyo wiki iliyopita kutoka Hospitali ya Mnazi mmoja iliyopo Visiwani Zanzibar.
Amesema upasuaji wa aina hiyo hawajawahi kuufanya hivyo basi baada ya majadiliano ya jopo la madaktari bingwa na kushauriana na mgonjwa waliona waufanye kwani kulikuwa na uwezekano mkubwa kwa mgonjwa kupona na kutoka katika maumivu makali aliyokuwa nayo.
Chanzo: HabariLeo
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.