RAIS Dkt. Magufuli ameahidi kuipatia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) shilingi bilioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za wafanyakazi ili kuwahakikishia makazi bora.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizindua majengo ya ofisi za TAKUKURU zilizojengwa eneo la Chikuyu B Wilaya ya Chamwino.
Aidha, Rais Dkt. Magufuli ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kutafuta eneo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa TAKUKURU.
Wakati huohuo, amewataka viongozi wa serikali kushirikiana na taasisi hiyo katika kupambana na rushwa nchini. “Wito kwa viongozi wa serikali kushirikiana na TAKUKURU. Wakuu wa mikoa na wakuu wa Wilaya wahakikishe wanatafuta majengo kwa ajili ya kujenga ofisi za TAKUKURU” amesema Rais, Dkt. Magufuli.
Katika hatua nyingine ameagiza mpango wa kujenga ofisi ya TAKUKURU wilayani Chato uhamishiwe Wilaya ya Kongwa.
Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la ofisi za TAKUKUTU wilaya ya Chamwino akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na viongozi wengine eneo la Chikuyu B Chamwino mkoani Dodoma jana.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.