RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli juzi tarehe 21 Februari, 2021 aliungana na waumini wa Parokia ya Mtakatifu Petro, Oysterbay Jijini Dar es Salaam kusali Misa Takatifu ya Jumapili (Dominika ya 1 ya Kwaresma) na alishukuru Watanzania kupitia Madhehebu yao ya Dini kwa kuitikia wito wa maombi ya kufunga ili Mungu aepushe ugonjwa wa Korona unaosababisha vifa vya watu duniani.
Mhe. Rais Magufuli alisema Wakristo ambao wapo katika kipindi cha Kwaresma na Waislamu ambao wanakaribia kuingia kipindi cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, waendelee kumuomba Mungu kwani pamoja na jitihada za kibinadamu za kukabiliana na ugonjwa huo, Mungu ndiye muweza wa yote na husimama kwa kila jambo.
Aliwataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Korona kama inavyoelekezwa na Wataalam wa afya na alifafanua kuwa Serikali haijazuia matumizi ya barakoa katika kujikinga kuambukizwa virusi vya Korona bali Watanzania wachukue tahadhari kwa kutumia barakoa zinazotengenezwa hapa nchini zikiwemoo za Bodi ya Dawa (MSD) au zinazotengenezwa na Watanzania wenyewe kwa kuwa barakoa zinazoingizwa kutoka nje ya nchi zina mashaka ya kuwa sio salama.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli alisisitiza kutumia njia za asili za kukabiliana na magonjwa ya kupumua ukiwemo ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kujifukiza (kupiga nyungu).
Mhe. Rais Magufuli amewataka Watanzania kuondoa hofu inayopandikizwa ambayo ina madhara ziadi, na amesisitiza kuendelea kumtumaini na kumtanguliza Mwenyezi Mungu kwa kuwa njia za kujikinga kwa barakoa, kutogusana na kutokaribiana (social distance) pamoja na kujifungia majumbani (lockdown) vimeonekana kutokuwa suluhisho la uhakika kwani Mataifa yanayofanya hivyo watu wake wanapoteza maisha kwa maelfu ikilinganishwa na hapa Tanzania.
Amempongeza Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro, Oysterbay Padre Dkt. Alister Makubi kwa mahubiri yaliyoeleza namna Yesu alivyojaribiwa na kwamba hata changamoto za sasa ikiwemo ugonjwa wa Korona ambayo yatapita.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.