RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Magufuli amewataka viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kusimamia ujenzi na upangaji wa Jiji ili kulinda hadhi ya Makao Makuu ya Nchi.
Agizo hilo amelitoa jana katika hotuba yake kabla ya kuweka jiwe la msingi jengo la makao makuu ya Idara ya Uhamiaji jijini hapa.
Dkt. Magufuli alisema “viongozi wa Dodoma endeleeni kusimamia vizuri ujenzi na upangaji wa Jiji la Dodoma”. Jiji la Dodoma ndilo Makao Makuu ya nchi, linatakiwa kupangwa vizuri ili liwe na hadhi ya makao makuu. Aidha, aliwataka viongozi hao kuwahimiza wananchi kupanda miti katika maeneo mbalimbali ili kutunza mazingira“. Dodoma ya kijani inawezekana” alisema Rais.
Rais aliipongeza Idara Uhamiaji kwa kazi nzuri. “Napenda kuipongeza Idara ya Uhamiaji kwa kazi nzuri na kupunguza kwa kiasi kikubwa nchi yetu kuwa kichochoro cha wahamiaji haramu”. Madhumuni na malengo makuu ya serikali kuhamishia makao makuu Dodoma ni kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi, miongoni mwa huduma ni zile zinazotolewa na Idara ya Uhamiaji, alisema. Aidha, alimtaka Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kuendelea kuwafuatilia watendaji wa Idara hiyo ambao wamekuwa wakitengeneza viza bandia na kuikosesha Serikali fedha ambazo zingeweza kutekeleza majukumu mengine.
Dkt. Anna nikuombe muendelee kufuatilia watendaji ambao wamekuwa wakitengeneza viza bandia na kuikosesha serikali fedha ambazo zingeweza kutekeleza majukumu mengine.
Vilevile, alitoa wito mkandarasi anayejenga jengo hilo, kampuni ya Suma JKT kukamilisha mradi huo kwa wakati. “Hakikisheni mnakamilisha ujenzi wa jengo hili, ikiwezekana hata kabla ya muda wenu kumalizika” alisema Rais Dkt. Magufuli.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.