Rais Dkt. John Pombe Magufuli jana Julai 15, 2019 amezindua rasmi huduma za tiba ya Saratani, upanuzi wa vyumba vya upasuaji, maabara ya kisasa ya Molecular Baiolojia, upanuzi wa jengo la wagonjwa wa dharura na mahututi, ufunguzi jengo la wagonjwa wanachama wa NHIF, mtambo wa kuzalisha Oksijeni ya wagonjwa na kiwanda cha kutengeneza maji ya mishipa ya damu (Dripu) katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza.
Aidha, Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kufanya utafiti ili kubaini sababu za wagonga wengi wa Saratani nchini kutokea mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Mapema akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando iliyopo jijini Mwanza, Prof. Abel Makubi amesema utoaji huduma ya mionzi kwa wagonjwa wa Saratani katika hospitali hiyo, umesaidia kuondoa adha kwa wagonjwa waliokuwa wakisafiri kwenda jijini Dar es salaam kusaka matibabu hayo.
Pichani Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando Baba Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza Renatus Nkwande pamoja na Mkurugenzi mkuu wa Hospitali hiyo Profesa Abel Makubi wakati akitoka kupata maelezo ya maboresho ya huduma za hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando ikiwemo huduma ya Tiba za Saratani pamoja na Kiwanda Kidogo cha Oxygen huduma ambayo inapatikana pekee katika hospitali hiyo.
Mwonekano ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya ziwa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.