Mgombea uras kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dkt. John Magufuli kujenga uwanja mkubwa wa michezo Dodoma utakaoweza kubeba wananchi wengi zaidi kwa wakati mmoja.
Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo katika hotuba yake ya uzinduzi wa kampeni ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo.
“Leo Dodoma imefurika, uwanja wa Jamhuri umejaa, lakini hata kule nje nako kumejaa. Hii inanipa changamoto kuwa nitakapochaguliwa kuwa Rais ni lazima nijenge uwanja mkubwa kuliko uliopo na hii itakuwa ndiyo kazi yangu ya kwanza. Dodoma ni Jiji, na leo mmefunga kazi, asanteni sana wana Dodoma. Hii inadhihirisha wazi kuwa hapa ni makao makuu ya nchi” alisema Dkt. Magufuli.
Aidha, Mhe. Magufuli alitaza ahadi zingine kuwa “Tumepanga kuongeza idadi ya watalii hadi kufikia Mil 5 2025, na mapato kutoka Dola Bil 2.6 hadi Dola Bil 6, tutapanua wigo wa vivutio vya Utalii, ikiwemo kukuza Utalii wa mikutano na uwindaji wa Wanyamapori na kuimarisha utalii wa fukwe,
Katika Awamu ya Pili tutahakiksha tunanunua Ndege zingine Tano, Moja ikiwa ya mizigo ambayo itakuwa ikienda moja kwa moja Ulaya,
Tutatengeneza nguo hapa Tanzania ili tuzivae wao tuwapelekee mitumba, tutatenga fedha za kuziandaa Timu zetu za Taifa,tutaweka mikakati ya kuwasaidia Wasanii ikiwemo kuwapa mikopo, hii michezo na sanaa tutavibeba, tutazidi kudhibiti rushwa na ufisadi,
Wataalamu wetu ambao wanaweza kutibu kienyeji watatambuliwa badala ya kupuuzwa,...,
Mliotutuma miaka 5 iliyopita tumeyafanya vizuri, tupeni tena miaka 5 mingine, tuendelee kuwa wamoja mambo mazuri makubwa yanakuja, tutaendelea kusimamia amani, umoja na mshikamano,tutaulinda Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar, tutakuza uchumi, tutapunguza riba kwenye Mabenki” alisema Dkt. John Pombe Magufuli.
Aidha, aliwataka watanzania kuendelea kumuomba Mungu ili azidi kuliongoza na kulisimamia Taifa la Tanzania liendelee kuwa na amani na umoja katika kipindi cha uchaguzi mkuu na baada ya uchaguzi mkuu.
Akimkaribisha mgombea urais kwa tiketi ya CCM, mgombea mwenza wa chama hicho, Mama Samia Suluhu Hassan, alisema kuwa serikali chini ya CCM imetekeleza kwa kishindo Ilani ya uchaguzi ya chama hicho. “Ndugu wananchi niseme, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita tumeweza kutekeleza kwa kishindo na tumeweza…Twende tukasonge mbele katika kampeni kwa heshima na kuomba kura kwa wananchi. Tukafanye kampeni kwa amani na kupiga kura kwa kishindo, tupate maeneldeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii” alisema Mama Samia.
Chama cha Mapinduzi kimezindua kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani katika uwanja wa Jamhuri jijini hap ana zitaendelea nchi nzima kwa takribani miezi miwili.
Maelfu ya wakazi wa Jiji la Dodoma waliofurika kushuhudia uzinduzi wa kampeni za mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi Jijini Dodoma leo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.