Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amekabidhiwa kijiti cha Uenyekiti wa SADC kutoka kwa aliekuwa Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Raisi Dkt. Hage Geingob wa Namibia katika Mkutano wa 39 wa Jumuiya hiyo ulioanza leo Jijini Dar Es Salaam.
Baada ya kupokea kijiti hicho, Rais Dkt. Magufuli amesisitiza mambo yafuatayo:
Ushirikiano - Amezitaka nchi mwanachama kushirikiana katika sekta zote ili kuhakikisha kuwa muungano huu wa SADC unawanufaisha wananchi wote wa nchi mwanachama ili kujiletea maendeleo.
Biashara - Amesisitiza kuwa ni vema nchi mwanachama zikashirikiana katika kununua na kuuziana bidhaa zinazopatikana ndani ya nchi za Jumuiya ya SADC ili kuimarisha uchumi wa mataifa mwanachama wa SADC.
Lugha ya Kiswahili - Amesisitiza matumizi ya Kiswahili ili kuwa na muungano shupavu utakaosaidia nchi mwanachama wa SADC kujitegemea kwa kila kitu ili kutoka kwenye utegemezi.
Rasilimali - Asema kwa upande wake ameona kuwa bado rasilimali za SADC hazijaisaidia Jumuiya hiyo kuwakomboa watu wake kiuchumi,asisitiza kuwa ni vema sasa jumuiya ikatumia rasilimali zake kuwaletea wananchi maendeleo.
Uwajibikaji - Asisitiza viongozi na wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kuletea mataifa yao maendeleo. Kila mtu awajibike kwa nafasi yake ili kuikomboa kiuchumi jumuiya hii.
Pia amesema atahakikisha kuwa anaitendea haki jumuiya hii kwa kuhakikisha kuwa anashawishi matumizi mazuri ya rasilimali za SADC katika kuwaletea watu maendeleo.
Viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika - SADC wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar Es Salaam.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.