MKURUGENZI wa kampuni ya John Snow Inc (J S I), Anthony Mwendamaka amekabidhi vifaa vya kuhifadhia taarifa za kitengo cha ustawi wa jamii katika Jiji la Dodoma ikiwa na lengo la kuimarisha mfumo wa utoaji huduma za afya ya jamii na ustawi wa jamii jijini humo.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za Jiji la Dodoma ambapo mwakilishi wa Mkurugenzi wa Jiji Dkt. Joseph Mdachi alipokea vifaa hivyo ikiwemo makabati 17 na fomu za kuhifadhia taarifa za walengwa ambao ni watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Mwendamaka alikabidhi vifaa hivyo vitakavyogawanywa katika kata15 za Jiji la Dodoma ili kusaidia utunzaji wa kumbukumbu na taarifa za ustawi kuanzia ngazi ya mtaa na Kata.
“Sisi kama kampuni ya John Snow Inc (J S I) tunahusika na research and Training tumekadhi vifaa yakiwemo makabati 17 fomu za kuhifadhia kumbukumbu za taarifa zitakazo kwenda katika kata 15 za hapa halmashauri ya Jiji la Dodoma”, Alisema Mwendamaka.
Alisema lengo la kuisadia Halmashauri ni kuimarisha mfumo wa utoaji huduma za afya na ustawi wa jamii kuanzia ngazi ya Kata hadi Wilaya ambapo taarifa za walengwa wanaopewa huduma za afya na ustawi wa jamii zinapaswa kuhifadhiwa sehemu salama.
Upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Joseph Mdachi aliipongeza taasisi hiyo kwa msaada wa vifaa hivyo na kutoa wito kwa wadau wengine wa sekta ya afya na ustawi wa jamii
kuendelea kuisadiana na Serikali kuimarisha mifumo wa utoaji wa huduma hizo kuanzia ngazi ya Mtaa, Kata na Wilaya kiujumla.
“Kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi, napenda kuwashukuru na kuwapongeza wadau hawa wa afya na ustawi wa jamii hapa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwani wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika kuhakikisha wanashirikiana na Serikali kuboresha huduma za afya na ustawi wa jamii kwenye Halmashauri yetu”, alisema Mdachi.
Makabidhiano hayo yalishuhudiwa na maafisa ustawi wa jamii ngazi ya Wilaya akiwemo mkuu wa kitengo hicho Halmashauri ya Jiji la Dodoma Rebeca Ndaki.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.