Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Angellah Kairuki amekutana na waheshimiwa Wabunge wa Jiji la Mwanza ili kuzungumza na kutatua changamoto katika Mkoa huo.
Kairuki amekutana na waheshimiwa Wabunge ikiwa ni muendelezo wa kazi anayoiendeleza ya kukutana na kusikiliza changamoto zinazowakabili kwenye maeneo yao.
Kairuki amekutana na Waheshimiwa Wabunge wa Jiji la Mwanza na watendaji wa Wizara ya OR-TAMISEMI ili kujua changamoto zinazowakabili katika Mkoa huo hasa katika Sekta ya Elimu, Afya na Miundombinu ya Barabara.
Lengo la kikao hicho ni kujenga ushirikiano kati ya Waheshimiwa Wabunge na Ofisi ya Rais - TAMISEMI ili kuzijua changamoto zilizoko kwenye maeneo yao na kuzitafutia ufumbuzi wa pamoja kwa kutambua kuwa Wabunge ni wawakilishi wa moja kwa moja wa wananchi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.