WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Angellah Kairuki amekutana na kufanya mazungumzo na Wabunge wa Majimbo na Viti Maalum wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kujadili Masuala mbalimbali anayotekelezwa na kusimamiwa Ofisi ya Rais TAMISEMI katika Mkoa huo.
Kikao hicho kilichofanyika tarehe 10 Novemba 2022 jijini Dodoma ambapo ni mwendelezo wa Vikao vya Waziri Kairuki Kukutana na makundi mbalimbali kujadili na Kuweka mikakati ya kutatua changamoto mbalimbali katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Wabunge wa Majimbo na Viti maalum katika Mkoa wa Kilimanjaro wakiongozwa na Mbunge wa Vunjo, Dkt. Charles Kimei wamepata wasaa wa kuwasilisha mapendekezo na changamoto mbalimbali na wamejadili mikakati ya kutatua na kuboresha baadhi ya masuala katika sekta za Elimu, Afya, Miundombinu ya barabara na Utawala bora.
Aidha, Wataalam kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Charles Msonde wametoa ufafanuzi wa hoja na hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali na Mipango iliyowekwa kutatua changamoto tofauti tofauti katika Mkoa Kilimanjaro.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.