WAZIRI wa Maji Mhe Jumaa Aweso na timu ya Wizara ya Maji pamoja na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) na
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wameshuhudia jitihada kubwa zinazoendelea kufanyika katika dhamira ya kuongeza hali ya upatikanaji wa Maji jijini Dodoma kwa kutembelea visima vikubwa vyenye Maji vilivyopatikana eneo la Nzuguni wakifatilia hatua kwa hatua kazi inayoendelea mpaka usiku bila kuchoka kwa nia ya kuona kazi inafanyika ili wanachi waweze kupata huduma bora ya Maji.
Katika ziara hiyo Kamati imeisisitiza Wizara ya Maji na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kumaliza kwa wakati au kabla ya wakati mradi wa maji unaotekelezwa katika Kata ya Nzuguni iliyoyopo jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma ametoa rai hiyo jana jijini Dodoma wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea mradi huo wa maji unaotarajiwa kuhudumia wananchi takriban 33,000 wa Mitaa ya Nzuguni, Ilazo na Kisasa.
Mhe. Dkt. Ishengoma amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuijali sekta ya maji na kujitahidi kutatua changamoto za maji hasa kwa wakati huu ambao miji mingi inakuwa na kusababisha ongezeko la watu.
Aidha, Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa maji uliopo Kata ya Nzuguni amesema;
“Leo tumetembelea eneo hili la Nzuguni ambalo wananchi wake walikuwa na changamoto kubwa ya maji, hatimaye tatizo hili linaenda kutatuliwa kupitia visima hivi vitano vilivyochimbwa vinavyotoa maji safi na salama yasiyo na chumvi.
Nawaomba sana mmalize mradi huu kabla ya miezi sita mliopanga ili wananchi wasiendelee kuteseka na kero hii”
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.