KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Bora na Serikali za mitaa (USEMI) ikiongozwa na Jaffari A. Chaurembo, Mbunge wa Jimbo la Mbagala imepokea na kujadili taarifa kuhusu Utekelezaji Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) katika halmashauri.
Kikao hicho kimefanyika Bungeni Jijini Dodoma tarehe 24 Oktoba, 2022 na kuhudhuliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Angellah Kairuki, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Dkt. Charles Msonde.
Kamati imepokea taarifa ya hali ya utekelezaji ujenzi wa shule mpya zinazojengwa kwa shilingi milioni 470 za awamu ya kwanza kwa kila shule ambazo zililenga kujenga miundombinu mbalimbali ya shule ikiwemo vyumba vya madarasa 8, maabara 3, jengo la utawala 1, Maktaba 1, Chumba cha TEHAMA 1 na matundu 20 ya vyoo vya wanafunzi pamoja na miundombinu ya kuvunia maji.
Mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) unalenga kuboresha elimu ya Sekondari na kutatua changamoto ya uhaba wa miundombinu ya shule ambapo mradi unatekelezwa katika eneo la Elimu ya Sekondari Kidato cha Kwanza hadi cha Sita kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2020/2021 hadi
2024/2025.
Aidha, Katika mwaka fedha 2021/2022 mradi umepeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya 235 za kata na shule 10 za wasichana za kitaifa katika mikoa 10.
Mradi wa SEQUIP unatekelezwa chini ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kufadhiliwa na Benki ya Dunia kwa mkopo wa Dola za Kimarekani Milioni 500 sawa na fedha za Tanzania kiasi cha Shilingi trilion 1.2.
Mikoa iliyowalisha taarifa za utekelezaji wa Mradi SEQUIP ni pamoja na Mikoa ya Kagera, Dodoma, Arusha, Morogoro, Katavi, Mara, Kilimanjaro na Pwani.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.