Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Dodoma mjini imefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo inayojengwa jijini hapa.
Ziara hiyo imeanza leo katika mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi cha mkoa kilichopo Nzuguni ambapo kamati hiyo ilipata maelezo juu ya hatua za ujenzi wa kituo hicho na kiwango ambacho ujenzi huo umefikia.
Aidha, kamati ya Siasa na Wilaya imetembelea mradi wa ujenzi wa Soko Kuu la Jiji eneo la Nzuguni, ambapo msafara wa kamati ya siasa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya Robert Mwinje walikuwa makini kwelikweli kusikiliza jinsi mradi huo utakavyokuwa na manufaa kwa wananchi pindi utakapokamilika mwezi Disemba 2019.
Kisha, msafara ulielekea eneo la Chinangari kutembelea mradi Eneo la kupumzikia (Recreational Pack) mradi huo utakupunguza msongamano mjini katika maeneo ya wazi kama Nyerere square. Mradi huo utakuwa na maeneo ya watoto kucheza na watu kupumzika, kufanya mazoezi, kwani kuna maeneo ya viwanja vya michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu, mpira wa pete, basketball, volleyball, na kadharika.
Mkuu wa msafara huo Mwinje ametoa ushauri kwa wananchi wa Dodoma kuitunza na kuijali miundombinu ya miradi yote inayojengwa, pia amewakumbusha wawekezaji waanze kuja kuwekeza kwenye miradi hiyo ili kujiingizia kipato kwani Dodoma limekuwa jiji kubwa.
Alimalizia kwa kuwapongeza Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mkuu wa mkoa, Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi wa jiji , wakuu wa idara, wakuu wa vitengo na watumishi wote wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kazi kubwa na nzuri wanazozifanya ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Aidha alipongeza juhud kubwa zinazofanywa na Mbunge, wenyeviti wa Kata na mitaa. Mwenyekiti huyo hakuacha kuwasifia na kuwahimiza wahandisi wa kapuni ya Mohamed builders kwa kazi nzuri wanazo zifanya ili lengo la kukamilisha miradi hiyo kwa uzuri na wakati linafikiwa.
Vile vile, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Patrobas Katambi amesema kuwa anamshukuru sana Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuri katika kuhakikisha anaifanya Dodoma kuwa ya thamani na yenye mvuto kwa kuipatia pesa nyingi ambazo zinasaidia kukamilisha miradi hii ya jiji.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.