HOSPITALI ya Benjamin Mkapa ikishirikiana na shirika la The One Heart Foundation Tanzania/USA imeandaa kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu kwa watoto wenye matatizo ya moyo itakayofanyika Septemba 26 hadi 30 mwaka huu hospitalini hapo.
Dkt. Rehema Yona Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto katika Hospitali ya Benjamin Mkapa ameeleza kuwa watoto watakao hudumiwa watawekwa katika makundi mawili yakihusisha waliokwisha fanyiwa uchunguzi na kugundulika na matatizo ya moyo na wale watakaofanya uchunguzi kwa mara ya kwanza.
“Wale watakaofika kufanyiwa uchunguzi kwa mara ya kwanza watawekwa katika mpango wa matibabu kulingana na matatizo yao unaoweza kuwa wa sasa au baadae, kwa wale waliokwisha gundulika na matatizo ya moyo tutawatibu moja kwa moja,” alisema Dkt. Rehema.
Dkt. Rehema aliongeza kuwa watoto watakaofanyiwa matibabu ni wale ambao wamezaliwa na matatizo ya moyo haswa wale wenye matundu kwenye moyo na wale ambao mishipa yao ya damu imebana hivyo kushindwa kusafirisha damu vizuri.
Kambi hiyo itashirikisha Madaktari Bingwa wa watoto na moyo kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma pamoja na Madaktari kutoka shirika la The one heart foundation.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.