Na. Shahanazi Subeti, DODOMA
Baraza la Madiwani wa Jiji la Dodoma wameipongeza Halmashauri ya Jiji chini ya Mkurugenzi na jopo lake kwa kutenga shilingi bilioni saba kwa ajili ya kumalizia miradi viporo na shilingi milioni 150 kwa kila kata kuanzisha miradi mipya ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
Madiwani waliyasema hayo katika mkutano maalum wa kupitia rasimu ya Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/2026 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe, alisema kuwa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/2026 ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma inalenga kukamilisha miradi viporo katika jumla ya kata 41 za halmashauri hiyo. “Kwa mwaka huu, Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma inafikia takribani shilingi Bilioni 147 inayolenga kwenda kukamilisha miradi viporo katika kata zetu 41. Miradi yote ambayo haikuisha kwa wakati kutokana na sababu zozote zile. Hivyo, tayari imetengwa kiasi cha shilingi Bilioni saba ili iweze kwenda kukamilisha hivyo viporo” alisema Prof. Mwamfupe.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Kilimani, Neema Mwaluko, alisema Mpango na Bajeti umekuwa ni mzuri sana na umelenga kwenda kuwasaidia wananchi wa kawaida ili kuwanyanyua kiuchumi. “Tukiangalia katika mpango huu na Bajeti, lengo mojawapo ni kumaliza viporo katika kata zetu. Mpango na Bajeti hii umekuwa ni mpango rafiki sana kwa mazingira ya kutoa huduma kwa wananchi wetu. Kwahiyo, naipongeza sana Timu ya Menejimenti ya Jiji ikiongozwa na mkurugenzi na Baraza la Madiwani” alisema Mwaluko.
Nae, Diwani wa Viti Maalum, Anna Mng’ong’o, alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa bajeti hiyo na kusema kuwa itasaidia kutatua matatizo katika kata na kuleta maendeleo. “Bajeti yetu ipo vizuri sana, bajeti hii imetenga shilingi Billioni 7, kwa ajili ya kumalizia miradi yote viporo katika Kata zetu. Tunaamini kwa Bajeti hii itaenda kujibu na kumaliza matatizo yote, hilo ni jambo la kujivunia sana” alisema Mng’ong’o.
Aidha, Diwani, Wendo Kutusha, alipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kufanya kazi kubwa katika kata kwa kutoa fedha kwa ajili ya maendeleo ya wananchi. “Kutengewa shilingi Milioni 150 kwa kila kata kwa ajili ya miradi ya maendeleo, sisi madiwani tunashukuru na tutahakikisha zinatumika kwa usahihi. Dodoma yetu itabadilika na litakuwa Jiji la mfano” alisema Kutush
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.