Na. Theresia Nkwanga, MIYUJI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameigusa Kata ya Miyuji kwa kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu na kuwapunguzia wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata elimu kwa kuwajengea shule mpya ya sekondari.
Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa Kata ya Miyuji, Beatrice Ngerangera mbele ya Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dodoma ilipofanya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Miyuji B.
Ngerangera alisema “Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameigusa Kata ya Miyuji kwa kutujengea shule mpya ya sekondari. “Kata ya Miyuji ilikuwa ikitumia shule ya Sekondari Miyuji iliyopo kata nyingine, tulikuwa tunanufaika lakini siyo kama tutakavyonufaika na shule hii. Tunamshukuru sana Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Shukrani kwa viongozi wa kata kwa ushirikiano tunaoupata mpaka hapa tulipofikia. Huu ni mradi mkubwa kwa sababu wanafunzi wanatembea zaidi ya kilometa tatu kufuata shule” alisema Ngerangera.
Shule ya Sekondari Miyuji ipo Kata ya Mnadani ambayo inahudumia wanafunzi kutoka Kata ya Mnadani na Kata ya Miyuji, ikiwa na idadi ya wanafunzi katika shule ya Sekondari Miyuji ni 1,467 kati yao wavulana ni 650 na wasichana ni 817 na ina walimu 65.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.