KATIBU Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amekutana na Balozi wa Ubelgiji nchini, Peter Huyghebaert kwenye Ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar Es Salaam.
Viongozi hao wamejadiliana masuala mbalimbali yakiwemo kuwawezesha Wananchi kiuchumi likiwemo kundi la Wanawake, kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia na Usawa waKijinsia.
Dkt. Chaula amemwambia Balozi Peter kuwa wananchi walio wengi wanaonesha utayari wa kujikwamua kiuchumi lakini tatizo linalowakabili ni zana na Technolojia duni ndio imekuwa changamoto ya kwenda mbele hivyo amemwomba Balozi huyo kuona uwezekano wa kuwezesha upatikanaji wa Technolojia hiyo kwa wananchi.
"Kuundwa kwa Wizara hii moja ya malengo yake ni kuwawezesha wananchi wetu waweze kujitegemea kiuchumi na wasimame wao wenyewe ili waweze kuchangia kwenye pato la Taifa kwa kulipa Kodi.
Kwa upande wake Balozi Peter Huyghebaert amesema Ubalozi huo upo tayari kuiwezesha Tanzania kupitia Programu zao mbalimbali katika kuhakikisha wananchi wanapata zana na Teknolojia bora zitakazowawezesha kujikwamua kiuchumi kwa kujiongezea kipato na kuchangia katika Pato la Taifa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.