HOSPITALI ya Rufaa ya KCMC ya Mkoani Kilimanjaro, imeanza rasmi kutoa huduma mpya za upandikizaji wa kioo cha mbele cha jicho ikiwa ni ya kwanza kufanyika miongoni mwa nchi za maziwa makuu na hivyo kurejesha matumaini kwa wagonjwa wa macho waliyopata athali kwenye kioo cha mbele cha jicho kuona tena.
Huduma hii imeanza kutolewa hospitalini hapo baada ya kupokea vifaa kutoka ughaibuni..
Akielezea zaidi daktari kutoka KCMC amesema kuwa zipo sababu nyingi zinazosababisha kioo cha mbele cha jicho (konea) kufa. Moja ya sababu hizo ni konea kupata kidonda na kinapopona huweka kovu sehemu ya kuonea na husababisha mtu kutoona. Tiba yake ni kuondoa kioo cha jicho chenye kovu na kuweka kipya.
Imeelezwa kuwa tayari wagonjwa 24 wameshapatiwa huduma hiyo ya awali na kuna uwezekano wa ongezeko kubwa la wagonjwa wa kupatiwa huduma hiyo siku za usoni.
Chanzo: azamtvtz (instagram)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.