Kichaa cha Mbwa ni ugonjwa wa kuambukiza unaoathiri mfumo wa kati wa fahamu yaani ubongo na Ugwe mgongo na kupelekea kupooza, kupoteza fahamu au kifo. Ugonjwa huu ni hatari na husabishwa na virusi viitwavyo kitaalam kitaalam kama rabies virus. Vijidudu hivi vinapatikana katika mate au damu ya binadamu na wanyama wengine kama mbwa, mbweha, paka, popo n.k.
Ufafanuzi huu umetolewa na Afisa Afya wa Jiji la Dodoma Abdallah Mahia leo alipokuwa akiongea na tovuti ya Jiji la Dodoma ili kutoa elimu na tahadhari kwa wakazi wa Jiji la Dodoma. Mahia amesema hatuna budi kuendelea kutoa elimu hii kwa wananchi wetu ili waweze kuchukua hatua mapema za kujikinga na madhara ya ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa. "Ugonjwa huu hauna msimu, wakati wo wote unaweza kutokea, hivyo ni muhimu kila mwana Dodoma kuchukua tahadhari ya kujikinga" amesema Afisa Afya wa Jiji la Dodoma.
Ugonjwa huu husambaa na kuleta madhara zaidi kwa watoto ndani ya muda mfupi chini ya siku 10. Hii hutokana na kinga yao kutokomaa, vilevile watoto huwa karibu sana na wanyama wafugwao na hivyo kupelekea kuumwa au kugusa mate yao.
Tiba yake mpaka sasa haijapatikana kama ilivyo kwa magonjwa mengine ya virusi lakini kumekuwepo chanjo ambayo hutolewa kabla au baada ya kuambukizwa ili kuzuia kusambaa na kuleta madhara mwilini. Pamoja na chanjo kama dalili zikiwa zimeshajitokeza kupona huwa sio rahisi.
Kwa takribani miaka 30 iliyopita ni watu 7 tu walipona baada ya chanjo wakiwa na dalili. Kuna mikakati iliyopo ya Umoja wa Kimataifa kuutokomeza ugonjwa huu ifikapo mwaka 2030.
Kutokana na hali ya kiuchumi nchi zinazoathirika zaidi ni za Africa, hii ndio sababu kubwa ikiwemo Tanzania kushindwa kutokomeza kichaa cha mbwa ambapo inakadiriwa gharama ya chanjo yake kufikia sh. 150,000.
Unaenezwa vipi kwa Binadamu:
Tofauti na mbwa ambaye amezoeleka kuambukiza ugonjwa huu, pia wanyama kama paka, mbweha, mbwa mwitu na popo wanahusishwa kwenye kuambukiza ugonjwa huu.
Dalili za Kichaa cha mbwa kwa binadamu
Dalili za ugonjwa huanza kuonekana baada ya mwezi hadi miezi mitatu baada ya kung’atwa na mnyama mwenye maambukizi, lakini pia tafiti zinaonyesha kuwahi hadi wiki tatu baada ya kuambukizwa hadi miaka saba.
Dalili hizi ni kama:-
Mara dalili hizi zinapoonekana maana yake ugonjwa umeshaanza kuharibu ubongo na neva na uwezekano wa mgonjwa kupona kunakuwa ni nadra sana na hivyo basi kifo huweza kutokea.
Matibabu na Kinga
Tiba ya chanjo kujikinga na maambukizi ya virusi hivi ikitolewa mapema au mara moja baada ya kuambukizwa, lakini tiba inahitaji kutekelezwa kabla virusi havijafikia ubongo, kwa hiyo ni muhimu kupata matibabu katika muda wa saa za kwanza baada ya kung’atwa.
Pia ni kutoa chanjo kwa mbwa wote ili kuwakinga na virusi hivi.
Ni muhimu wanyama wa kaya wapewe chanjo dhidi ya ugonjwa huu ili kulinda mbwa kutopata maambukizi ya virusi hivi.
Kuosha mahali palipo umwa au penye mchukubo kwa dakika 15 kwa maji na sabuni au povidoni/iodine, vinaweza kuua virusi pia na kuwa na ufanisi fulani katika kuzuia maambukizi ya kichaa cha mbwa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.