MGANGA Mkuu wa Manispaa ya Musoma Dkt. Mustafa Waziri amesema kituo cha Afya Makoko kimefanikiwa kufanya upasuaji kwa mara ya kwanza leo Novemba 8, 2022.
"Upasuaji umefanyika kwa dakika 50 kuanzia saa 5: 40 hadi 6:30 jioni chini ya madaktari na wauguzi na kufanikisha kuzaliwa mtoto wa kiume mwenye uzito wa kilo 3.5."amesisitiza Dkt. Waziri
Amesema ni historia ya pekee kwa kituo cha Makoko tangu kuanzishwa kwake na ni faraja kubwa kufanya upasuaji kwa kuwa ilikuwa ndoto ya muda mrefu kwa kituo hicho.
Dkt Waziri amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa fedha anazoendelea kutoa ambapo fedha hizo zimenunua vifaa ambavyo vimetumika na nyingine kuongezewa na fedha za Mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo.
Kituo cha Makoko ni Moja ya vituo vitatu vya Afya vilivyo chini ya mamlaka ya Halmashauri ya Manispaa ya Musoma vituo vingine ni Nyasho na Bweri na kinatarajiwa kuhudumia zaidi ya wakazi 10, 000.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.