KITUO kikuu cha mabasi cha Dodoma kinatarajia kuanza kutoa huduma siku chache zijazo baada ya kukamilika ujenzi wake katikati ya mwezi Februari, 2020.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu kukamilika kwa zoezi la ujazaji wa fomu za maombi ya maeneo ya biashara katika kituo kikuu cha mabasi cha Dodoma na soko kuu la Job Ndugai leo.
Kunambi ameseme “kituo kikuu cha mabasi cha Dodoma kitaanza kazi muda mfupi kuanzia sasa kama Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli alivyoelekeza”. Amesema kuwa mchakato wa maombi na nafasi za kufanya biashara katika kituo kikuu cha mabasi Dodoma na Soko kuu la Job Ndugai umekamilika.
Mkurugenzi wa Jiji amewataka wafanyabiashara wote waliofaulu kupata nafasi za biashara kufuatilia majina yao katika tovuti ya Halmashauri ya Jiji (www.dodomacc.go.tz) na mbao za matangazo ili waweze kuchukua fomu za masharti ya upangaji katika maeneo ya biashara.
Mkurugenzi Kunambi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo katika Jiji la Dodoma zaidi ya shilingi trilioni moja.
Ikumbukwe kuwa ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi Dodoma kimegharimu kiasi cha shilingi bilioni 24 na soko kuu la Job Ndugai limegharimu shilingi bilioni 14.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.