KIKOSI cha Dodoma Jiji kimewasili salama Jijini Mbeya na leo asubuhi kimefanya mazoezi ya mwisho katika dimba la Sokoine Jijini humo ikiwa ni mazoezi ya mwisho kabla ya kuwakabili Mbeya City siku ya kesho tarehe 09.03.2021 saa 10:00 katika dimba hilo.
Timu ya Dodoma Jiji FC inamiikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma wakati Mbeya City FC inamilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya hivyo timu zote kuwa chini ya himaya ya Halmashauri za Majiji, ikumbukwe katika Ligi Kuu ya Vodacome Tanzania timu nyingine inayomilikiwa na Halmashauri ni KMC inayomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati timu hiyo ikifanya mazoezi Kocha Mkuu Mbwana Makata amesema kuwa Mbeya City ni timu nzuri ambayo imekua ikicheza mpira mzuri licha ya kutopata matokeo katika mechi za hivi karibuni hivyo wataingia kwa tahadhali kubwa ili waweze kupata matokeo katika mchezo huo.
“Kila timu huwa ngumu inapokua katika uwanja wake wa nyumbani hivyo hata Mbeya City sio timu ya kubeza inapokua nyumbani tutapambana kuhakikisha tunashinda katika mechi hii ili tuzidi kujihakikishia nafasi ya kusalia katika tano bora ya Ligi Kuu Tanzania Bara” Alisema Makata.
Aidha Makata amesema kuwa kikosi chake hakina majeruhi yeyote jambo ambalo litampa yeye wigo mpana wa kupanga kikosi chake ili aweze kuondoka na pointi tatu muhimu.
Timu ya Dodoma Jiji FC imecheza michezo 22 ya Ligi Kuu, ikikusanya pointi 32 huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi kukamilisha duru la 23.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.