MCHEZO wa Ihefu dhidi ya Dodoma Jiji leo umemalizika kwa Dodoma Jiji kupoteza mchezo huo kwa kufungwa goli moja bila kwa mkwaju wa penati ambayo imelalamikiwa vikali na wadau wa soka kutokana na penati hiyo kuwa na ukakasi huku refa akiyakataa magoli mawili halali yaliyofungwa na Dodoma Jiji.
Akizungumza baada ya mchezo huo Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji FC Mbwana Makata ameonesha kutoridhishwa na vitendo vya mwamuzi wa mchezo huo ambae alionekana kuegemea upande wa Ihefu ambao wapo kwenye hatari ya kushuka daraja.
Makata amesema kuwa wachezaji wake walikua kwenye kiwango kizuri na walistahili kushinda mchezo huo lakini maamuzi ya mwamuzi wa mchezo huo yameamua matokeo na kuwapatia wapinzani wao ushindi.
“Naweza kusema kuwa kinara wa mchezo wa leo alikua ni mwamuzi kutokana na maamuzi yake kwani kama angechezesha kwa haki tungeshinda mchezo huo kwasababu amekataa magoli yetu mawili ya wazi na kuwapa Ihefu penati ambayo kimsingi beki wangu hakuunawa mpira uliopelekea yeye kuwazawadia wapinzani wetu penati” aliongeza Makata.
Wakati huo huo, timu ya Dodoma Jiji inatarajia kurejea Makao Makuu wa Nchi kujiandaa na mchezo wao wa kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Simba katika dimba la Mkapa Jijini Dar es salaama siku ya tarehe 26-05-2021.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.