• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Kongamano la Rushwa latoa matumaini ya kuendelea kutokomeza Rushwa nchini

Imewekwa tarehe: July 10th, 2025

Na. Nnacy Kivuyo, DODOMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amesema Tanzania inaendelea kufanya vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa kila mwaka kutokana na utawala bora uliopo nchini.

Aliyasema hayo wakati akifungua Kongamano la Maadhimisho ya siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika yaliyofanyika jijini Dodoma.

Alisema kuwa kuanzishwa kwa Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ndani ya Mahakama Kuu pamoja na Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2023 ni hatua nyingine muhimu katika kuhakikisha vitendo vya rushwa vinadhibitiwa ipasavyo nchini.  “Ndugu washiriki, Tanzania imepiga hatua kubwa katika jitihada za kutokomeza rushwa, ikiwa ni pamoja na kutunga na kufanya maboresho ya sheria mbalimbali zinazolenga kupambana na vitendo hivyo. Tuendelee kuzitumia sheria hizi sambamba na kutoa elimu ili kuhakikisha wananchi wanafahamu nafasi na wajibu wa kila mmoja katika kuitokomeza rushwa” alisema Waziri Simbachawene.

Aidha, alitoa maelekezo Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuongeza kasi katika utekelezaji wa majukumu yake ili kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa nchini. “Ndugu washiriki, natoa wito kwa TAKUKURU na wadau wote kutengeneza mbinu mpya ambazo hazijazoeleka ili kusaidia kuboresha mapambano dhidi ya rushwa. Ni jukumu letu kuangalia namna taasisi zetu zinavyohudumia wananchi, kwasababu huduma bora na haki ni kipimo  cha mafanikio yetu” alielekeza Waziri Simbachawene.

Nae,  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Chrispin Chalamila alisema kuwa mapambano dhidi ya rushwa yatachangia katika kukuza heshima ya binadamu ambayo mara nyingi hupokwa na vitendo vya rushwa. “Katiba ya Jamhuri ya Muungao wa Tanzania ya 1977 katika Ibara ya 8 (1) (b) inatamka kuwa lengo kuu la serikali ni ustawi wa wananchi, Katiba hiyo pia katika Ibara ya 9 (h) inaitaka serikali na taasisi zake kuhakikisha kuwa vitendo vya rushwa na aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini. Majadiliano kuhusu rushwa yanayofanyika katika maadhimisho haya yatasaidia kukuza heshima ya binadamu hapa nchini na barani Afrika” alisema Chalamila.

Alimalizia kwa kusema kuwa jitihada za kuendelea kuimarisha mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa zitachangia kufikia lengo la serikali la kuleta ustawi wa jamii ya watanzania na kukuza heshima ya ubinadamu.

Kwa upande mwingine, Mkurugunzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa uchumi Zanzibar (ZAECA), Ali Abdalla Ali alisema kuwa maadhimisho hayo yatasaidia kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutojihusisha na vitendo vya rushwa na uhujumu uchumi nchini. “Kongamano hili la mapambano dhidi ya rushwa, linazikumbusha taasisi zinazoratibu mapambano dhidi ya rushwa katika nchi wanachama wa umoja wa Afrika kulinda utu na haki za kila mtu ili kuimarisha utawala bora” alisema Ali.

Maadhimisho hayo yaliongozwa na kaulimbiu isemayo “Kukuza na kulinda heshima ya binadamu katika mapambano dhidi ya rushwa” ikizikumbusha taasisi zinazoratibu mapambano dhidi ya rushwa katika nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kulinda utu na haki za kila mtu ili kuimarisha utawala bora.






Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Shekimweri: Maafisa tarafa na Watendaji wa kata zingatieni Maadili na Uwajibikaji

    July 23, 2025
  • Serikali yatoa bilioni 298 kugharamia matibabu ya Kifua kikuu, Ukimwi na Malaria nchini

    July 22, 2025
  • Ushirikiano kati ya tanzania na canada waipaisha sekta ya afya

    July 21, 2025
  • Vifaa vya kupima maji vitumike mara baada ya mafunzo

    July 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.