• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Kongole Jiji Dodoma kwa Hati Safi – RC Mtaka

Imewekwa tarehe: June 19th, 2021

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

MWAKILISHI wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Nathalis Linuma amepongeza ushirikiano wa Baraza la Madiwani na Menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliopelekea kupata hati safi ya ukaguzi wa hesabu za serikali.

Kauli hiyo ameitoa leo katika mkutano maalum wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupitia na kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa hesabu za Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2020 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Linuma alisema “nilipopitia taarifa hii, nimeona hoja za Halmashauri ya Jiji la Dodoma hazipo vibaya. Hoja nyingi siyo za kupelekea kupata hati mbaya. Katika kipindi hicho, Halmashauri ya Jiji la Dodoma pekee ndiyo ilipata hati safi kati ya halmashauri nane za Mkoa wa Dodoma. Naomba nichukue nafasi hii kulipongeza sana Jiji la Dodoma. Tulipata hati safi yenye msisitizo. Matokeo haya yanatokana na mshikamano mzuri baina ya Baraza la Madiwani na Menejimenti ya halmashauri”.

Aidha, aliwataka madiwani wa halmashauri hiyo kuendelea kusimamia vizuri taratibu za fedha ili kuiepusha halmashauri kupata hati chafu. Aliwakumbusha kuwa wajibu wao wa msingi ni kuwasimamia wataalam ili wazingatie sheria, taratibu na kanuni katika kutekeleza majukumu yao.

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe alipongeza maoni mazuri ya wajumbe katika kuboresha utendaji kazi wa halmashauri. “Maoni mazuri hayana mwisho, yatusaidie kuifanya kesho yetu iwe bora kuliko leo. Kukosoana kwa kujenga ni maendeleo. Hakulengi sura ya mtu, bali kunalenga tabia. Tuendee hivyo, ili kuwa Makao Makuu ya nchi kiwe kielelezo cha utendaji kazi” alisema Prof. Mwamfupe.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alisema kuwa Halmashauri yake ndiyo pekee iliyosalimika na kupata hati safi kati ya halmashauri nane za mkoa wa Dodoma. “Sababu kubwa ni kutokana na kufanya kazi kwa uadilifu, nidhamu na kutii maelekezo ya viongozi ambayo waheshimiwa madiwani ndiyo viongozi wenyewe” alisema Mafuru. Aidha, aliahidi kuendelea kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na viongozi kwa lengo la kuhakikisha halmashauri yake inaendelea kupata hati safi.

Akiwasilisha taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kwa hesabu za Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2020, Mweka Hazina wa jiji hilo, CPA Rahabu Philip alisema kuwa hoja zote zimejibiwa na kuwasilishwa kwa Mkaguzi wa Nje ndani ya siku 21. Alisema kuwa taarifa hiyo inaonesha kuwa halmashauri ina jumla ya hoja 63 kwa mwaka 2019/2020. Katika hoja hizo, 29 ni za miaka ya nyuma na 34 ni hoja za mwaka 2019/2020.

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru akizungumza kabla ya kuwakaribisha wajumbe wa Baraza maalum la Kujadilia Hoja za mkaguzi mkuu wa Serikali.

Akiwasilisha taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG)

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.