KUVUNJWA kwa iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) na majukumu yake kuchukuliwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kumesaidia kupunguza kero za upatikanaji wa viwanja na kusogeza huduma kwa wananchi kwa haraka.
Kauli hiyo ilitolewa na Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Mlima wa Moto Assemblies of God, Silvanus Damiano Komba hivi karibuni jijini hapa.
Mchungaji Komba alisema kuwa aliwahi alienda kufuatilia kiwanja kwa iliyokuwa CDA kwa miezi mitatu bila mafanikio. “...na kwa kuwa niliwahi kwenda CDA kushughulikia kiwanja miezi mitatu sikufanikiwa na nikasema kwa kweli sitarudi tena CDA. Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Joseph Magufuli kuivunja ile CDA na majukumu yake kuchukuliwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Nimekwenda kwa mara ya kwanza baada ya kuwa Jiji wiki iliyopita, nataka niwaambie watu wote mliokuwa na habari mbaya ya CDA, sasa hivi Jiji limebadilika” alisema Mchungaji Komba.
Huduma zimeboreka sana katika Halmashauri, aliongeza. “Namshukuru Mungu kwa Mkurugenzi wa Jiji na Maafisa Ardhi wote waliopo pale Jiji. Nimefika Jiji ndani ya masaa mawili tumefanikiwa kupewa eneo la kujenga kanisa eneo ya Mtumba” alisema Mchungaji Komba kwa furaha.
“Mungu ambariki Mkurugenzi wa Jiji, Mungu awabariki maafisa ardhi wateule, kwakuwa nilibahatika kuyajua hata majina, mmoja anaitwa Kamonga na mmoja anaitwa Mutalemwa, walinishughulikia kwa kiwango cha juu mpaka niliogopa!!” aliendelea kusema Mchungaji Komba.
"Nimeshangaa, mahali ambapo watu walikuwa wanakaa mwaka mzima, ndani ya masaa mawili! Jiji limebadirika, Mungu ambariki Mkurugenzi wa Jiji hili, awabariki Maafisa Ardhi Wateule Kamonga na Mtalemwa walinishughulikia kwa kiwango cha juu mpaka niliogopa!" alisema Mchungaji Komba kwa hisia.
Mchungaji huyo alisema kuwa awali alidhani kahudumiwa kutokana mwili wake na umbile lake na nafasi yake na umbile lake. “Nilifikiri kwa sababu ya mwili wangu, umbile langu au cheo changu, lakini nyuma yangu alifuata bibi kizee mmoja, naye alishughurikiwa kwa namna isiyo ya kawaida! Leo nasimama tena hapa kuibariki Jiji, wabarikiwe katika kazi zote” alibariki.
Akiongelea ubabaishaji katika huduma, alisema kuwa hakuna longolongo wala rushwa. “Na ramani tumepata, ni eneo kubwa na ingekuwa zamani hapa ni mamilioni ya shilingi. Lakini tutatakiwa kulipa million nne tu” alisema Mchungaji huyo.
Aidha, Mchungaji Komba alimpongeza Rais Magufuli kwa kuivunja CDA na kumteua Mkurugenzi mahiri na ambaye anafanya kazi kwa hofu ya Mungu. Mwishoni alimpongeza Mstahiki Meya ambaye alimuona akiwahudumia wananchi wanyonge ofisini kwake.
Jiji la Dodoma linaendelea na mkakati wake kuhakikisha linamaliza migogoro yote iliyokuwepo na kutekeleza kwa ufanisi majukumu yake ikiwemo kutoa huduma kwa wananchi wa Dodoma pamoja na kuendelea na ujenzi wa Makao Makuu ya Nchi yetu kwa ustawi wa Tanzania.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.