HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imepongezwa kwa jinsi inavyotekeleza miradi ya kimkakati katika jitihada zake za kusogeza huduma karibu na wananchi na kukuza uchumi wa Jiji hilo.
Pongezi hizo zilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Mhandisi Mshamu Munde baada ya kukamilika kwa ziara kutembelea miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma jana katika soko kuu la Ndugai linalojengwa jijini hapa.
Mhandisi Munde alisema kuwa lengo la ziara hiyo na timu yake ya wataalam ni kujifunza na kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati. “Tumejifunza sana, nashukuru wataalam wa Halmashauri ya Jiji hili mmetutembeza na kutueleza kwa kina namna mnavyotekeleza miradi hii. Siwezi kusita kutoa pongezi kwa namna miradi hii inavyotekelezwa na pia inavyosimamiwa. Ushirikiano tumeona ni mkubwa. Hata wasilisho tulilopewa ofisini lilikuwa fasaha” alisema Mhandisi Munde.
Aidha, alionesha kuridhishwa na ushirikishwaji wa wataalam katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati. “Jambo ambalo naona ni la kujivunia na kulichukua kwa sisi kama Halmashauri ambao tutatekeleza miradi kama hii kwa baadae ni ushirikishaji wataalam. Hili ni jambo muhimu sana. Unajua kama mradi huufahamu vizuri hata usimamiaji wake unakuwa hafifu” alisisitiza kwa furaha.
Miradi yote tuliyotembelea inaubora unaokubalika na imezingatia thamani ya fedha, aliongeza.
Wakiwa Jijini Dodoma wataalam hao walitembelea ujenzi wa miradi ya kimkakati ya kituo cha kuegesha malori cha Nala, Kiwanda cha kutengeneza matofali-Low cost, kituo kikuu cha mabasi Dodoma na soko kuu la Ndugai.
Kituo Kikuu cha Mabasi ni moja na miradi ya kimkakati ya Jiji la Dodoma kilichotembelewa na timu ya wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Mshamu Munde.
Eneo la kuegesha malori lililopo Nala ni miongoni mwa miradi ya kimkakati iliyotembelewa na kusifiwa na timu ya wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.