Na. Dennis Gondwe, DODOMA
MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri amelipongeza Jiji la Dodoma kwa ukusanyaji mzuri wa mapato ya ndani na kushauri vyanzo vyote vya mapato vikubwa vitambuliwe na kuwekewa mikakati ya ukusanyaji.
Pongezi hizo alizitoa alipoongoza Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Dodoma maalum kwa ajili ya kujadili rasimu ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Jiji.
Shekimweri alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma inafanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato. “Niwapongeze kwa ukusanyaji mapato. Karibia kila mwaka Halmashauri ya Jiji la Dodoma mnavuka lengo la makusanyo ya mapato. Rai yangi ni vema kwenye bajeti yenyewe mkatuambia ni vipi vyanzo vikubwa mnavyovitegea kwenye mapato. Vyanzo vikubwa viwekewe mkakati wake na kuteua Meneja wa kusimamia mapato kwenye vyanzo hivyo. Wawekeeni malengo ya makusanyo na motisha wakifikia malengo hayo” alisema Shekimweri.
Aidha, alishauri halmashauri kufanya ulinganifu wa gharama zinazotumika kukusanya mapato na kile kinachokusanywa. “Ni vema mkawa na ulinganisho wa gharama ya kufuatilia chanzo cha mapato na mapato yanayopatikana. Lazima tujiulize kama chanzo kinatuletea shilingi 200,000 lakini gharama ya kufuatilia hayo mapato ni shilingi 2,000,000 kuna haja ya kuangaika nacho?. Lakini chanzo kinakuletea shilingi 50,000,000 ukitumia shilingi 1,000,000 mimi nakuelewa” alisema Shekimweri.
Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imekadiria kukusanya na kutumia mapato yenye jumla ya shilingi 128,278,555,369 kutoka vyanzo katika vyanzo vyake vya ndani, serikali kuu, wahisani kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo, utoaji huduma na kujiendesha.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.