Waheshimiwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo wamekula kiapo mara baada ya kuanza kwa Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge la 12 Bungeni Jijini Dodoma.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambaye pia ndiye Mkurugenzi wa kwanza kuongoza Jiji la Dodoma Mhe. Godwin E. Kunambi (pichani), Mbunge wa Jimbo la Mlimba mkoani Morogoro alikuwa miongoni mwa wabunge hao walioapa mbele ya Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai. Kunambi ameacha historia katika Jimbo la Dodoma kwa kuliongoza kwa mafanikio makubwa Jiji hilo hasa katika ukusanyaji mapato ya ndani, usimamizi wa ardhi, upimaji na ugawaji wa viwanja na pia uibuaji na utekelezaji wa miradi ya kimkakati.
Tovuti hii inamtakia kila la heri katika utekelezaji wa majukumu yake kama Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.