MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amepongezwa kwa kutetea haki za Wananchi wanyonge na kuwafanya kuendelea kuwa na imani zaidi na Serikali ya awamu ya tano katika kutatua kero.
Pongezi hizo zimetolewa na mkazi wa mtaa wa Mtakuja Bi. Amina Hamisi (99) wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Dkt. Binilith Mahenge ya kusikiliza kero za Wananchi juu ya migogoro ya Ardhi katika Kata ya Chang’ombe Jijini humo jana Februari 13, 2019.
“Mimi natoa pongezi kwa kazi nzuri inayofanywa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kutetea wanyonge… aliwatuma wathamini kupima eneo langu kwa ajili ya kuanza ujenzi kufuatia mgogoro uliokuwepo katika kiwanja hicho na kuutatua”.
Bi. Amina ambaye pia ni mnufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini (TASAF) alipongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano kwa Wananchi wake.
“Natoa pongezi kwa Serikali ya awamu ya tano kwa kuwa na mpango wa TASAF kwani umetusaidia Wananchi masikini na kuacha kwenda kuomba pesa katika uwanja wa Nyerere ‘square’ siku hizi” alisema Bibi huyo.
Katika ziara hiyo ya kusikiliza kero za Ardhi kwa wakazi wa mtaa wa Mtakuja, Mkuu wa Mkoa aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Kunambi, Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mhe Anthony Mavunde, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi na Maafisa waandamizi wa serikali.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.