MKURUGENZI wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi amewatahadharisha wananchi wa Kata ya Mtumba katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma kuwa makini na makampuni yanayokuja kinyemela kupima na kuuza ardhi bila idhini ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji.
Kunambi ameyasema hayo kwenye mkutano wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mhe. William Lukuvi na Wananchi wa Kata ya Mtumba, ambapo alitoa ufafanuzi juu ya suala la upimaji na ulipwaji fidia wa eneo lililotwaliwa kwa ajili ya ujenzi wa Mji wa Serikali.
"Kuna matatizo yamewakumba wenzetu wa maeneo mengine kama Dar Es Salaam, kuna ujanja wa makampuni ya upimaji wanakuja kimya kimya kwenye mitaa, wanakuja na ramani walizoziandaa wenyewe bila ya Mamlaka husika kujua, na sisi Dodoma lazima tuwatahadharishe Wananchi wetu" alisema Kunambi.
(Tembelea facebook yetu: Dodoma Jiji, Tufuatilie twitter: @DodomaJiji, Subscribe Youtube: Dodoma City TV)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.