WATOTO wanne wamepoteza maisha Mkoani Dodoma baada ya kuzama kwenye maji kwa nyakati tofauti.
Mtoto mmoja alizama kwenye maji wakati akiogelea ,mwingine akiwinda bata maji kwenye mabwawa huku wawili wa familia moja wakifariki dunia baada ya kutumbukia kwenye kisima cha maji ambayo yalikuwa ni kwaajili ya matumizi ya nyumbami.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo,Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Gilles Muroto amesema matukio hayo yametokea katika maeneo tofauti,hivyo ametoa wito kwa wananchi kuwa makini na watoto wao kwa kuwakataza kwenda katika maeneo hayo ambayo yamekuwa yakitumika kwaajili ya kuogolea na kuvua samaki.
‘’tumeshapoteza vijana wanne kwa matukio ya kuogelea kwenye maji,tarehe 26/4/2021 kijiji cha mkoka kata ya Nzoisa mtoto Kanduru Kasakama (9) alizama maji wakati akiogolewa na wenzake,mwingine 25/4/2021 kata ya mlali mtoto kulwa Jakson simango (15) alizama maji wakati anawinda bata maji wakati akiwinda na wenzake na 25/4 /2021 kata Nzoisa watoto wa familia maji Samora Amos (6) na Emanuel Amosi (13) walizama kisimani baada ya kutumwa na mama yao kwenda kuchota maji kwaajili matumizi ya nyumbani’’Amesema muroto
Wakati huo huo amesema jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 41 wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo wizi wa pikipiki 16 na kumkamata Bwana Charles (30 ) kwa makosa ya kumiliki silaha aina ya Shot Gun isivyo halali.
‘’Maeneo ya Nkuhungu,Chang’ombe,Airport ,Nzuguni,Area c na Swaswa ,kwahiyo tumekamatwa karibia pikipiki 16 na watuhumiwa 41 ambao wanajihusisha na vitendo vya uhalifu’’Amesema Muroto
Akizungumzia Mkutano Mkuu wa chama cha Mapinduzi unaotarajiwa kuanza April 29-30 ,Kamanda Muroto amesema jeshi la polisi limeendelea kujiimarisha kuhakikisha kuwa wageni wote wanaokuja kuhudhuria katika mkutano huo wanakuwa salama huku likitoa onyo kwa matapeli.
‘’Kuna wale wanaojifanya maafisa usalama wa Taifa hiki ni kipindi ambacho mara nyingi huwa wanajipenyeza na kufanya matukio hayo,hao wote tutakuwa tunawachunguza" alisistiza Kamanda huyo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.