WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua tawi la benki ya Mwanga Hakika jijini Dodoma na kuitaka benki hiyo iwe kimbilio la wajasiriamali na wakulima wadogo.
“Kuweni kimbilio la wajasiriamali na wakulima wadogo. Njooni na bidhaa na vivutio muhimu kwa makundi hayo ya wajasiriamali na wakulima wadogo. Hilo ni kundi ambalo linahitaji zaidi huduma zenu katika kuliwezesha kujikwamua kiuchumi,” amesema.
Ametoa wito huo leo (Jumanne, Agosti 31, 2021) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali, wanahisa na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa tawi la benki ya Mwanga Hakika (Mwanga Hakika Bank) jijini Dodoma.
Waziri Mkuu ameitaka benki hiyo ipunguze riba ili kuendana na dhamira ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye amekuwa akilisemea suala hilo mara kwa mara. “Nanyi pia lizingatieni hili katika kukua kwenu kwani kupungua kwa kiwango cha riba kutasaidia kusisimua biashara na shughuli nyingine za kiuchumi,” amesisitiza.
Aidha, ameitaka benki hiyo iongeze ubunifu. “Kuweni wabunifu. Sambamba na kutengeza faida, kuongeza amana za benki na kutoa gawio kwa wanahisa, njooni na ubunifu utakaoboresha huduma zenu na kuzifanya kuwa ubora zaidi, zenye tija na gharama nafuu kwa walaji.”
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.