KAMATI ya Kudumu ya Bunge, Utawala na Serikali za Mitaa pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa wameipongeza Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kuanzisha Mfumo wa Usimamizi wa Mikopo ya Asilimia 10
Hayo yamesemwa leo Oktoba, 27, 2022 na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa
Benaya Kapinga Mbunge wa Mbinga Vijijini kwenye mafunzo ya kujengewa uwezo kuhusu matumizi ya mfumo wa Usimamizi wa Mikopo ya Asilimia 10 yaliyofanyika bungeni Jijini Dodoma.
Amesema kuwa mfumo huo utasaidia kusimamia utoaji, urejeshaji na usimamizi wa mikopo inayotolewa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, jambo ambalo litasaidia kupata taarifa sahihi za utoaji na urejeshwaji wa mikopo inayotolewakwa wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum.
"Hili jambo tulikuwa tukilitolea maelekezo kuitaka Serikali kuanzisha mfumo utakaosaidia kujua hali halisi ya mikopo iliyotolewa, iliyorejeshwa na ambayo haijarejeshwa ili kupunguza kasi ya wanaokopeshwa kutorejesha mikopo hiyo kwa wakati au kutorejesha kabisa jambo ambalo huleta hasara kubwa kwa Serikali" amesisitiza Kapinga
Aidha, wameiomba Serikali kuhakikisha inatoa elimu kwa jamii hasa kwa wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum ambao ndio walengwa wakuu kuhusu mfumo huo ili kuwajengea uwezo na uelewa wa kutumia mfumo katika uombaji na urejeshwaji wa mikopo
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki amezishukuru kamati hizo kwa kutoa mchango na kutumia weledi katika kuishauri na kuisimamia Serikali lengo ikiwa ni kutoa maboresho katika utendaji kazi
Aidha amesema Serikali itaendelea kubuni Mifumo itakayorahisisha utendaji kazi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na kuhakikisha mifumo hiyo inazungumza na niendelevu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.